CAF Champions League

WYDAD AC YAWASILI KUIKABILI SIMBA TANZANIA.

Published on

Klabu ya Wydad AC tayari imewasili nchini kwaajili ya mchezo wake wa nne wa hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya Simba utakaopigwa Jumanne wiki ijayo.

Wydad AC inazisaka alama katika mchezo huu kwa udi na uvumba kwani ndizo zitakazowapa mwanga kama timu hiyo itafuzu hatua ya robo fainali.

Huu ni mchezo wa kwanza wa Wydad AC wataenda kucheza bila kocha wake mkuu Adil Ramzi ambaye amefutwa kazi siku chache zilizopita kutokana na kupata matokeo yasiyoridhisha.

Huu utakuwa ni miongoni mwa michezo migumu zaidi kuwahi kuchezwa baada ya kila timu kuhitaji kupata alama mhimu.

Hadi hivi sasa Simba ina alama mbili [2] pekee ilizozipata baada yakutoka sare na Asec Mimosas [Nyumbani], Jwaneng Galaxy [Ugenini], na imepoteza mchezo mmoja dhidi ya Wydad AC [Ugenini], ipo mkiani mwa msimamo wa kundi B.

Wydad AC hadi hivi sasa ina alama tatu [3] ilizozipata baada ya kushinda mchezo mmoja [1] dhidi ya Simba [Nyumbani], imepoteza michezo miwili [2] dhidi ya Jwaneng Galaxy [Nyumbani], Asec Mimosas [Ugenini], ipo nafasi ya tatu [3] ya msimamo.

Kundi B hadi hivi sasa linaongozwa na Asec Mimosas yenye alama Saba [7], nafasi ya pili ni Jwaneng Galaxy alama nne [4], Wydad AC nafasi ya tatu alama tatu [3] na Simba inaburuza mkia na alama mbili [2].

Popular Posts

Exit mobile version