International Football

AL AHLY KUWAVAA MAN CITY?

Published on

Klabu ya soka ya Al Al Ahly ya nchini Misri leo itamenyana na timu ya Fluminense ya nchini Brazili kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Kombe La Dunia la Vilabu yanayofanyika nchini Saudi Arabia.

Itakumbukwa kuwa Al Ahly wanaingia Hatua hiyo baada ya kuwaondosha Al Ittihad ya Saudi Arabia baada ya kuwanyuka mabao 3-1.

Endapo Al Ahly watawaondosha Fluminense basi watacheza mchezo wa Fainali dhidi ya mshindi wa mechi kati ya Urawa Reds mabingwa wa Asia watakaomenyana na mabingwa wa Ulaya, Manchester City mtanange unaotarajiwa kupigwa kesho Jumanne ya tarehe 19 Disemba 2023.

Popular Posts

Exit mobile version