Kocha mkuu wa klabu ya Medeama ya nchini Ghana Evans Augustin amelalamika kuwa wamenyimwa uwanja wa kufanyia mazoezi tangu wamefika hawajafanya mazoezi.
“Tangu tumekuja tumeshindwa kufanya mazoezi, tunajikuta tunafanyia mazoezi hotelini.
“Tumekosa uwanja wa kufanyia mazoezi sijajua ni kwanini, ila hii ni changamoto ambayo tumekutana nayo ila sijui kwanini tumekosa, zipo ishara zinazoonyesha kuwa tumenyimwa”.
- amesema Kocha Mkuu wa Medeama SC, Evans Augustin.
Huu utakuwa mchezo wa pili kwa timu hizi kukutana baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Ghana kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1.
Goli la Yanga lilifungwa na kiungo nyota na hatari Pacome Zouzoua na kwa upande wa Medeama lilifungwa na Christian Sowah kwa mkwaju wa Penalty.
Medeama itacheza na Yanga kesho kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.
Mchezo huu utatoa mwanga kwa klabu ya Yanga kama itakuwa na matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.