Nyota wa klabu ya Yanga raia wa Ghana, mshambuliaji fundi Hafidhi Konkoni amejumuishwa kwenye kikosi cha awali cha timu ya Taifa ya Ghana kitakachoelekea nchini Ivory Coast kwaajili ya fainali za mataifa ya Afrika mwezi January.
Kikosi hicho cha wachezaji 53 kitafanyiwa mchujo tena na kupatikana wachezaji 27 pekee watakaoiwakilisha Ghana katika fainali za mataifa ya Afrika mapema mwezi January nchini Ivory Coast.
Konkoni amekuwa hana wakati mzuri sana kwenye kikosi cha Yanga tangu alipojiunga nacho mapema mwanzoni mwa msimu huu kwenye dirisha kubwa la usajili.