Uongozi wa klabu ya Simba umewasimamisha wachezaji wawili [Clatous Chama na Nassor Kapama] kwasababu ya utovu wa nidhamu.
Nyota hao sasa watafikishwa kwenye kamati ya nidhamu ya klabu hiyo ili swala lao lijadiliwe na hatua zaidi za kinidhamu zichukuliwe.
Hivyo nyota hao hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho katika michezo ijayo hadi pale kamati ya nidhamu itakapotoa hukumu yake.
Klabu ya Simba imewataka wachezaji na wafanyakazi wa klabu hiyo kufuata misingi ya klabu hiyo na kutokuvunja sheria na kanuni za klabu bali wazingatie utendaji kazi.
Hata hivyo Mwamba wa Lusaka Clatous Chama mkataba wake na klabu ya Simba utafika tamati mwishoni mwa msimu huu na Simba haina mpango wa kumuongezea mkataba hivyo ataondoka kama mchezaji huru.