Rais wa shirikisho la soka Barani Ulaya Aleksander Ceferin amewapa uhuru wa kuendelea na Ligi ya European Super League huku akisubiri kuona kama Ligi hiyo itaweza kufanikiwa kwa kushirikisha timu mbili pekee.
Kwa upande mwingine Ceferin amesema ameona mashabiki wa soka England wakiifananisha Ligi ya ESL kama Ligi ya Mazombie.
“Natumaini wataanza kucheza Super Leage yao haraka iwezekanavyo, na klabu mbili”.
“Hatutajaribu kuwazuia kabisa. Wanaweza kutengeneza chochote wanachotaka, acheni wafanye, tuna mpango wetu”.
“Natumaini wanaelewa nini wanachokifanya, elewa kwamba mpira wa miguu sio kwaajili ya biashara”.
“Nimeona mashabiki wa England wakiita LIGI YA MAZOMBIE”.
“Ni karibu na Christmas, wameona box chini ya mti na wakasherehekea, lakini hata hivyo walipofungua hilo box wakagundua kuwa hapakuwa na vitu vingi ndani”.
Mapema leo mahakama ya usuluhishi imetoa mamlaka kwa European Super League kuanzishwa baada ya hapo awali kuzuiliwa.
Klabu nyingi kubwa Barani Ulaya zimetangaza kutoshiriki Ligi hiyo ikiwemo, Manchester United, Bayern Munich, PSG, Villareal, Sevilla, Juventus na zingine nyingi.
Klabu hizo zote zimetoa waraka kila timu kwa kwakati wake, jambo ambalo linampa kujiamini zaidi Rais wa UEFA Ceferin kuwa mashindano haya hayatafanikiwa.
Ni klabu mbili tu ambazo hadi hivi sasa ziko tayari kushiriki, Real Madrid na FC Barcelona zote za nchini Hispania.