Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeondoka leo kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Timu ya taifa ya soka ya visiwani humo, Zanzibar Heroes.
Mchezo huo unaotarajiwa pia kuwa maalumu kwa ajili ya kuuzindua uwanja wa Amaan uliokuwa kwenye kukarabati mkubwa hivi karibuni, Unatarajiwa kupigwa Jumatano ya tarehe 27 Disemba, 2023.