EPL

VARANE KUTIMKIA BAYERN MUNICH•

Published on

Bayern Munich wanapanga kutaka kumsajili Raphael Varane kutoka Manchester United na wako tayari kulipa kiasi cha Euro milioni 20 (£17m/$22m) kwa ajili ya beki huyo.


Bayern wanatumai kuimarisha safu ya beki wa kati katika dirisha la usajili la Januari na wameweka malengo yao kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ili kumuongezea machaguo kocha Thomas Tuchel, Sport inaripoti. Miamba hao wa Ujerumani pia wamekuwa wakihusishwa na beki wa Barcelona Ronald Araujo, lakini raia huyo wa Uruguay hana mpango kuhama Januari.


Kumekuwa na mazungumzo ya uwezekano wa uhamisho wa Varane baada ya kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United, huku Harry Maguire, Jonny Evans na Victor Lindelof wakipewa nafasi ya kucheza badala yake.

Varane, ambaye alishinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa alijiunga na United akitokea Real Madrid mnamo Agosti 2021 na mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu.

Amecheza mechi 10 za Premier League msimu huu, akiwa amerejea kwenye kikosi cha kwanza kwa mechi za hivi majuzi dhidi ya Liverpool na Aston Villa.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anaweza kuhusika katika michezo ya Ligi Kuu nchini Uingereza (EPL) iliyosalia katika mwaka huu wa 2023 dhidi ya Nottingham Forest kabla ya kuanza kufikiria uwezekano wa kuhamia Bayern Munich.

Popular Posts

Exit mobile version