NBC Premier League

SINGIDA FG HAINA URAFIKI NA MAKOCHA.

Published on

Timu ya Singida Fountain Gate FC) imeachana na kocha wao mkuu Heron Ferreira aliyedumu kwa miezi miwili tangu mwezi wa kumi tarehe 15 baada ya kuachana na Mjerumani, Ernst Middendorp ambae aliikimbia timu ya Singida FG FC baada ya kuingiliwa majukumu yake kwa kupangiwa Kikosi.

Singida Fountain Gate FC imeachana na Heron Ferreira pamoja na wasaidizi wake, ambapo akiwa Singida Fountain Gate, Ferreira ameiongoza Singida katika michezo tisa ya ligi akishinda minne, sare tatu na kupoteza miwili ameiacha ikiwa nafasi ya tano na alama 20.

Singida Fountain Gate ilianza msimu na Kocha Hans Van Plujm ambae alitimuliwa akaja Mjerumani Ernst Middendorp na baadae Heron Ferreira kabla ya kutimuliwa.

Heron Ferreira sifa yake kubwa kudumu na timu moja kwa zaidi ya miaka miwili, mara nyingi kwenye CV yake amedumu na timu miezi sita, muda mwingi aliokaa na timu moja ni mwaka mmoja tu.

Heron Ferreira ndani ya miaka kumi (10) amefundisha timu nane (9), Kazi yake ya mwisho alikuwa kocha mkuu wa Al Merreikh ambapo aliajiriwa November 14 mwaka 2022 na akatimuliwa April 23, mwaka 2023.

2014- ASA FC
2015- ISMAILY
2016- AL AHLY SHENDI
2017- BONSUCESSO
2019- AL AHLY SHENDI
2020- NAJRAN SC
2020- ISMAILY
2023- AL MERRIKH SC
2023- SINGIDA FG FC (MIEZI 2).

Popular Posts

Exit mobile version