Makala Nyingine

ANCELOTTI AIKACHA BRAZIL, ANASALIA MADRID.

Published on

Rais wa shirikisho la soka nchini Brazil Ednaldo Rodrigues Gomes mapema mwaka huu alitangaza kuwa kocha Carlo Ancelotti atajiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil kuwa kocha mkuu kuelekea mashindano ya CONMEBAL pindi mkataba wake na Real Madrid utakapotamatika.

Mkataba wa Real Madrid na Carlo ulitarajiwa kuisha mapema mwakani [2024] lakini cha kushangaza leo klabu hiyo imemuongezea mkataba wa miaka miwili hadi 2026 wa kuendelea kusalia kikosini hapo.

Carlo ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa ana furaha sana baada ya mkataba huo mpya na anaona watafikia malengo makubwa zaidi.

“Leo ni siku ya furaha sana, mimi na Real Madrid tunaendelea kuwa pamoja katika kutafuta mafanikio mapya na makubwa, Shukrani kwa kila mmoja na Hala Madrid”.

Popular Posts

Exit mobile version