Klabu ya Arsenal imewasilisha malalamiko yake kwa waamuzi nchini England [PGMOL] wakilalamika kuwa nyota wao Bukayo saka anafanyiwa madhambi ya makusudi mara nyingi.
Arsenal inahitaji nyota huyo alindwe awapo uwanjani, Bukayo saka ni mchezaji wa tatu kwa kufanyiwa madhambi mara nyingi [87] nyuma ya Jordan Ayew [117] na Bruno Guimaraes [92].
Mwanzo klabu ya Arsenal iliwasilisha malalamiko yake ikiwataka marefa kuongeza umakini wawapo uwanjani baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Newcastle.