Jadon Sancho yuko tayari kukwepa jinamizi linalo muandama katika klabu yake ya Manchester United, huku jaribio lake la kutaka kurejea kwa mkopo Borussia Dortmund kuripotiwa kukubaliwa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, ambaye alihamia Old Trafford kwa pauni milioni 75 ($95m) msimu wa joto wa 2021, amejikuta akizuiliwa kuitumikia Manchester United katika msimu wa 2023-24. Akiwa ameshutumiwa na Erik ten Hag kwa kuruhusu kiwango kushuka katika mazoezi, Sancho hajaitumikia United tangu Agosti 26 na amelazimika kufanya mazoezi na kikosi cha watoto (akademi) ya timu hiyo.
Njia ya kuondoka imepatikana katika dirisha la usajili la Januari. Inadaiwa kuwa Sancho atarejea Ujerumani kwa mkataba wa muda mfupi ambao utagharimu Dortmund pauni milioni 2.6 tu na kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuanza tena kucheza mpira katika mazingira aliyoyazoea.
Inaelezwa kwamba maelezo machache ya kodi yanahitajika kutatuliwa kabla ya Sancho kuwa huru kuondoka Manchester United, ikiwezekana kwamba anaweza kujiunga na Dortmund kwenye kambi yao ya majira ya baridi ya Marbella siku ya Ijumaa – kabla ya BVB kupata tarehe ya mchezo wa kirafiki na AZ. Alkmaar siku ya Jumamosi.
Sancho alifunga mabao 50 na pasi za mabao 64 akiwa na Dortmund katika mechi 137, kabla ya kupachika mabao mengine 12 na kutoa pasi 6 za mabao katika mechi 82 za United, huku akitokea benchi mara tatu mwanzoni mwa msimu huu.