Pambano la masumbwi kati ya Anthony Joshua na Francis Ngannou tayari limepangwa kufanyika na tarehe itapangwa mapema mwezi huu Jijini London, England.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa na mizunguko kumi, baada ya pambano hilo kutangazwa AJ alisema atalimaliza pambano hilo kwa KO “Knock Out”.
Baada ya kauli hiyo Ngannou akasema
“Tyson Fury alisema hivyo pia na Tyson Fury ni bora kuliko Anthony Joshua”.
Pambano la Anthony Joshua na Francis Ngannou litafanyika nchini Saudi Arabia. Hili litakuwa ni pambano la pili kwa Francis Ngannou raia wa Cameroon kupigana rasmi tangu alipoanza mapambano ya Boxing.
Pambano la kwanza lilikuwa dhidi ya Tyson Fury ambalo lilipigwa nchini Saudi Arabia, Pambano hilo lilifuatiliwa na watu wengi zaidi Duniani, zaidi Barani Afrika na kushuhudiwa Fury akishinda kwa alama, jambo ambalo liliwashangaza wengi walioamini Ngannou alistahili ushindi.