AFCON

STARS YAWASILI KIBABE AFCON, MASHABIKI WAIPA UBINGWA.

Published on

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” tayari imewasili nchini Ivory Coast ikitokea nchini Misri ambako ilikuwa imeweka kambi ya maandalizi kwaajili ya fainali za mataifa ya Afrika “AFCON 2023”.

Tanzania imewasili nchini Ivory Coast ikiwa na idadi ya wachezaji 27 waliosajiliwa kwaajili ya michuano hiyo huku watatu [3] wakiwa sehemu ya wachezaji wa akiba ambao ikitokea mmoja majeruhi basi wanachukua nafasi yake.

Mashabiki wengi wa Tanzania kila mmoja kwa wakati wake amekuwa akizungumza vitu chanya kuhusu kikosi hicho kinachonolewa na kocha raia wa Algeria Adel Amrouche hasa kutokana na mabadiliko aliyoyafanya kwenye kikosi hicho.

“Point tatu [3] kwa Zambia Point tatu [3] kwa DR Congo halafu Morocco tuna droo sisi hao robo fainali” Alisema Shabiki mmoja.

“Siku zote tumekuwa tukipoteza wachezaji wetu wengi sana wenye asili ya hapa huko ughaibuni. Lakini kwa sasa pongezi nyingi kwa kuwasaka huko walipo na kuwarejesha nyumbani ili walipambanie taifa lao” Shabiki mwingine aliongeza.

Mara ya mwisho kikosi cha Taifa Stars kushiriki michuano hii ilikuwa mwaka 2019 ambapo kiliondoshwa kwenye hatua ya makundi bila kupata alama yoyote huku wakifunga magoli mawili [2] pekee.

Msimu huu Taifa Stars imeelekea nchini Ivory Coast ikiwa na wachezaji wengi wapya ambao wamepata nafasi kwa mara ya kwanza kuvaa jezi ya timu ya Taifa ya Tanzania kwenye michuano hii mikubwa Barani Afrika.

Kuelekea michuano hii kocha mkuu wa Stars Adel Amrouche aliwahi kunukuliwa akisema “michuano hii itamfanya kiungo Feisal Salum na mlinzi Ibrahim Hamad Abdullah waonekane zaidi kutokana na ubora walionao”.

Taifa Stars ipo kundi moja na timu za Taifa za Morocco, Zambia na DR Congo huku mchezo wake wa kwanza unatarajiwa kuchezwa January 17 dhidi ya Morocco.

Popular Posts

Exit mobile version