Makala Nyingine

HENRY AMEISHI NA MSONGO WA MAWAZO MUDA MREFU.

Published on

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa Thierry Henry ameweka wazi kuwa amekuwa akiishi na tatizo la msongo wa mawazo kwenye maisha yake yote ya soka.

Henry amesema kuwa hakutaka kuruhusu jambo hilo limsumbue sana kwake lakini alichoamua kufanya ni kuendelea kufanya kile anachokiamini.

“Kwenye maisha yangu yote ya soka na tangu nazaliwa, nimekuwa kwenye msongo wa Mawazo”.

“Nilikuwa najua ? Hapana. Nilifanya kitu kuhusiana na hilo ? Hapana. Lakini niliendana na hiyo hali”.

Unatakiwa kutanguliza mguu mmoja mbele, kisha mguu mwingine ili utembee ndio kitu ambacho nilikuwa naambiwa tangu nikiwa mtoto”.

“Sijawahi kuacha kutembea labda ningetambua”.

Msimu wa 2002/03 akiwa na Arsenal alicheza michezo 55, akafunga magoli 32 na kutoa pasi za usaidizi wa magoli 28, anatajwa kuwa alikuwa miongoni mwa washambuliaji hatari zaidi Duniani.

Thiery Henry aliifungia klabu yake ya Arsenal magoli 174 hadi hivi sasa akisalia kuwa kinara wa magoli kwenye kikosi hicho, na magoli 42 kwente mashindano ya Ulaya.

Popular Posts

Exit mobile version