AFCON

NIGERIA YAONGEZA MSHAMBULIAJI MWINGINE.

Published on

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Nigeria Jose Peseiro amemjumuisha kikosini mshambuliaji wa klabu ya OGC Nice ya Ufaransa Terem Moffi akichukua nafasi ya Victor Boniface.

Victor Boniface aliumia jana kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Guinea uliomalizika kwa kipigo cha goli 2-0.Takwimu zake msimu huu, mechi 23, Goli 16 na pasi za usaidizi wa magoli nane [8].

Terem Moffi hadi hivi sasa ameitumikia timu ya Taifa ya Nigeria michezo 12 akifunga goli nne [4]. Msimu huu akiwa na Nice amecheza mechi 17 akifunga goli sita [6] na pasi za usaidizi wa magoli mbili [2].

Popular Posts

Exit mobile version