Ligi kuu ya soka la Wanawake Tanzania Bara, WPL imeendelea leo kwa viwanja viwili tofauti kuwaka moto.
Huko mkoani Dodoma, Yanga Princess walikuwa wakimenyana na wenyeji wao Fountain Gate Princess kwenye dimba la Jamhuri mkoani humo na wageni kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Bao pekee la mchezo huo lilipatikana dakika ya 38 ya mchezo kupitia kwa Arin Madarina n kudumu kwa dakika zote 90.
Kwa Matokeo hayo Yanga Princess wanafikisha alama 9 baada ya mechi 4 wakijizatiti kwenye nafasi yao ya 3 wakiwa nyuma ya Simba na JKT Tanzania kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa lakini wakiwa na michezo mkononi.
Kwingineko huko Mkoani Iringa, kwenye dimba la Samora, CEASIAA walitoshana nguvu na Bunda Queens kwa kutoka suluhu ya 0-0 wakiwa nyumbani.
Matokeo hayo yanazifanya timu zote 2 kubaki kwenye nafasi zao, Bunda Queens nafasi ya 6 na CEASIAA wakibaki nafasi yao ya 7 wote wakiwa na alama 4 wakipishana kwenye magoli ya kufunga na kufungwa.