NBC Premier League

SINGIDA FG YASHINDWA KUNSAJILI BANDA, ATIMKIA KMC.

Published on

Klabu ya KMC imeinasa saini ya nyota wa zamani wa klabu ya Simba Peter Banda raia wa Malawi. Peter Banda unakuwa ni usajili mwingine mkubwa ambao KMC wameufanya kwenye dirisha hili dogo la usajili ambalo litafungwa siku mbili zijazo.

Awali nyota huyo alihitajika na klabu ya Singida Fountain Gate lakini.mazungumzo hayakuenda kama ambavyo walikusudia na mwisho wa siku ofa ya KMC ikamvutia zaidi na huenda hivi karibuni akatangazwa kwenye klabu ya KMC.

Nyota huyo raia wa Malawi msimu uliopita alikuwa anaitumikia klabu ya Nyasa Big Bullet ya nchini kwao Malawi, urejeo wa Peter hapa nchini unaweza kumpa nafasi ya kuonekana zaidi kwa mashabiki zake.

Mashabiki wa soka nchini kila mmoja amekuwa na maoni yake kuhusu urejeo wa nyota huyu wa zamani wa klabu ha Simba.

“Kijana ni kipaji sahihi, lakini majeruhi yalimuathiri sana”, shabiki mmoja alizungumza.

“Simba ilikuwa na wachezaji wazuri waliokosa nafasi na muda tu, Simba ina presha kubwa sana kuliko uwezo wake, huko kwingine hakuna presha atafanya vizuri”, shabiki mwingine alieleza.

Hata hivyo klabu ya Singida Fountain Gate imefungiwa kufanya usajili wa nyota wa kimataifa na kitaifa kutokana na adhabu waliyopewa na shirikisho la soka Duniani baada ya kushindwa kuwalipa wachezaji wake wa zamani.

Adhabu ya Singida Fountain Gate itamalizika pindi tu itakapo kamilisha malipo ya nyota wao wa zamani, kwasasa haiwezi kufanya maingizo ya nyota wapya ikiwemo Peter Banda.

Popular Posts

Exit mobile version