Klabu ya Barcelona haiwezi kufanya usajili wa nyota yoyote kwenye dirisha hili dogo la usajili kutokana na sheria ya matumizi ya pesa kupita kiasu, Financial Fair Play [FFP].
Baada ya kupoteza mchezo wa jana mbele ya Real Madrid [4-1] taarifa kadhaa zilisambaa zikihusisha Xavi kuachana na kikosi cha Barcelona lakini mtendaji mkuu wa Barcelona Deco amekanusha taarifa hiyo.
“Financial Fair play ina athiri klabu nyingi sana na hatuwezi kukamilisha sajili yoyote kwa sasa, huo ndio ukweli”.
“Xavi hajakalia kuti kavu na kazi yake haipo mashakani, ni upuuzi tu. Sisi wote hapa Barcelina tuna mwamini Xavi, kiukweli”.
“Tumeshasema kufungwa mara moja hakuwezi kupoteza au kututoa kwenye mipango yetu”, Amesema mtendaji mkuu wa Barcelona, Deco.
Kwasasa Barcelona haitafanya usajili wa maingizo ya nyota wapya kutokana na sheria ya matumizi ya pesa kupita kiasi na bado wanaandamwa na majeruhi mengi kwenye kikosi chao.
Asilimia kubwa ya nyota wanaotumika na kikosi cha Barcelona kwasasa ni vijana kutoka kwenye Academy ya Lamasia kutokana na nyota wengi wa kikosi cha kwanza kupata majeraha.