17:00 Burkina Faso vs Mauritania.
Hizi ni dondoo mhimu kuelekea mchezo wa mapema hii leo wa fainali za mataifa ya Afrika kati ya Burkina Faso dhidi ya Mauritania.
• Burkina Faso kuelekea mchezo huu hadi hivi sasa katika michezo mitano [5] iliyopita wameshinda mechi tatu [3], wamepoteza moja [1] na kutoa sare mechi moja [1].
• Mara ya mwisho timu hizi mbili kukutana Burkina Faso aliibuka na ushindi wa goli 2-1, magoli ya Burkina Faso yakifungwa na nyota wa Yanga Stephen Aziz Ki na Konate, huku goli pekee la Mauritania likifungwa na Ibnou Ba.
• Katika michezo mitano iliyopita Burkina faso wamefunga magoli tisa [9] na wameruhusu magoli matano [5].
• Mauritania katika michezo mitano [5] ya mwisho wameshinda mchezo mmoja [1] pekee, wamepoteza michezo miwili [2] na wametoa sare michezo miwili [2].
• Mauritania wamefunga magoli matatu [3] wamefungwa magoli matano [5].
• Nyota wa kuchungwa zaidi kwa upande wa Mauritania ni mshabuliaji wa Hemeya Tanjy na Sheikh El Welly anayekipiga US Monastr.
• Aziz Ki ndiye nyota wa kuchungwa zaidi kwenye mchezo wa Leo anayekipiga kwenye klabu ya Yanga ya Tanzania.