Match : Tunisia vs Namibia .
Uwanja : Amadou Gon Coulibaly.
Mji : Korhogo, Ivory Coast.
Timu ya Taifa ya Tunisia itashuka dimbani kwenye mchezo wake wa kwanza wa fainali za mataifa ya Afrika kuikabili timu ya Taifa ya Namibia.
- Tunisia katika michezo mitano [5] iliyopita ameshinda michezo mirltatu [3], imepoteza mchezo mmoja [1] na kutoa sare mchezo mmoja [1].
- Mara ya mwisho Tunisia kupoteza mchezo ilikuwa dhidi ya Japan walipokubali kichapo cha goli 2-0.
- Kwenye michezo mitano iliyopita Tunisia imefunga magoli saba [7] na imefungwa magoli mawili [2].
- Katika michezo mitano [5] iliyopita Namibia imeshinda mchezo mmoja [1], sare tatu [3] na imepoteza mchezo mmoja [1].
- Mara ya mwisho Namibia kupoteza mchezo ilikuwa dhidi ya Equatorial Guinea walipo chapwa goli 1-0.
- Namibia katika michezo mitano [5] ya mwisho, imefunga magoli mawili [2] na imeruhusu goli moja [1].
- Kwa takwimu hizi Namibia imekuwa timu ngumu sana kuruhusu magoli na kufunga pia lakini Tunisia ina ukuta imara na inafunga sana magoli, hii ni moja ya mechi bora sana kuitazama.
- Tunisia ipo nafasi ya 28 kwa ubora Duniani, na Namibia ipo nafasi ya 115 kwa ubora Duniani.