AFCON

MASHABIKI WALITAKA SHIRIKISHO KUMPA TIMU MGUNDA.

Published on

Shirikisho la soka nchi Tanzania TFF limemteua aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania Hemed Suleiman “Morocco” kuwa kaimu kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania akisaidiwa na Juma Mgunda.

Hii inakuja baada ya kocha mkuu wa kikosi hicho kufungiwa na shirikisho la soka Barani Afrika “CAF”, kibarua cha kwanza kwa Hemed na Mgunda kitakuwa jumapili hii dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia.

Wadau wa soka nchini kila mmoja kwa wakati wake wametoa maoni yao baada ya kocha mkuu kufungiwa na timu kukabidhiwa Hemed Suleiman na Juma Mgunda.

“Kocha anayefuata awe Juma Mgunda, hiyo ni mashine ya boli litembee sio kuzuia tu kama kocha aliepita, safari hii hatutaki makocha wa kigeni tuwaamini wazawa ndo wana uchungu na Taifa”, Alisema shabiki mmoja.

“TFF msizunguke sana timu mpeni Juma Mgunda halafu muandalieni vijana wa kutosha, tunavipaji vingi mno hapa Bara na Visiwani”.

“Chukueni hawa vijana pelekeni ufaransa, Hispania, Ureno halafu andaeni Academy imara kama tatu, muone kama 2027 hatufiki Robo fainali”, maoni ya mdau mwingine wa soka nchini.

“Matumaini ya kuwapiga chipolopolo na wacongomani yapo hapa”, Alisema shabiki mwingine wa Stars.

Taifa Stars ina kibarua kizito kwenye mchezo unaotarajiwa kufanyika kesho Jumapili dhidi ya Zambia, kama itapoteza basi safari ya kurudi nyumbani itawadia na kama ikiibuka na ushindi itakuwa na matumaini ya kusonga hatua ya 16 bora.

Kila la kheri makocha wetu mliopewa dhamana na kila lahkeri Taifa Stars watanzania wapo pamoja na nyinyi licha ya kupoteza mchezo wa kwanza lakini imani juu yenu ni kubwa sana.

Popular Posts

Exit mobile version