Kocha mkuu wa Equatoria Guinea Juan Micha ameweka wazi kuwa presha kubwa kwenye mechi ya leo ipo upande wa mwenyeji Ivory Coast na hivyo watautumia mwanya huo kufanya jambo.
Micha ameweka wazi kuwa leo watawaondoa wenyeji wa mashindano hayo kwenye uwanja wao wa nyumbani mbele ya mashabiki zao.
“Itakuwa mechi ngumu kwa timu zote lakini zaidi kwa Ivory Coast kwasababu wanahitaji ushindi, tutauendea mchezo huu kwa utulivu”.
” Hatutasubiri, tunajua watatushambulia na kutaka kutufungua, kitu ambacho tutakitumia kuwashangaza kwenye uwanja wao wenyewe”.
“Tunajua wapo kwenye presha kubwa kuliko sisi”, Juan Micha kocha mkuu wa Equatorial Guinea.
Ivory Coast wana alama tatu [3] wakiwa nafasi ya tatu [3] ya msimamo wa kundi A na leo watacheza mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya kinara wa kundi hilo Equatorial Guinea aliye na alama nne [4].
Mchezo huo utapigwa saa mbili [20:00] usiku wa leo.