AFCON

GHANA YATIMUA BENCHI ZIMA LA UFUNDI TIMU YA TAIFA.

Published on

Shirikisho la soka nchini Ghana limetangaza kuachana na kocha wake Chris Hughton baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya AFCON inayoendelea nchini Ivory Coast.

Ghana imepata alama mbili pekee kwenye kundi lake baada ya kutoa sare michezo miwili na kupiteza mchezo mmoja huku ikishika nafasi ya tatu ya msimamo wa kundi.

Taarifa kutoka shirikisho hilo zinasema pia limefuta benchi zima la ufundi na siku zijazo litatangaza mwelekeo mpya wa benchi la ufundi.

“Shirikisho la soka nchini Ghana linapenda kuwatangazia kuwa limeachana na kocha wa timu ya Taifa ya Ghana Chris Hughton kuanzia sasa”.

“Mamlaka pia zimechukua maamuzi ya kuachana na benchi zima la ufundi la Black Stars”.

“Shirikisho la soka Ghana litatangaza mwelekeo wa baadae wa benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Ghana”, Taarifa kutoka shirikisho la soka Ghana.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa timu ya Taifa ya Ghana kuondolewa kwenye hatua ya makundi kwenye fainali za mataifa ya Afrika.

Popular Posts

Exit mobile version