Makala Nyingine

KUELEKEA MCHEZO WA NAMIBIA vs MALI.

Published on

Dauda Sports inaelezea jinsi azma ya Namibia kutinga hatua ya 16 bora ya Afcon watakapocheza na Mali (The Eagles) leo Jumatano.

Namibia inatazamia matokeo hayo ya ushindi na kutinga hatua ya mtoano kutoka Kundi E watakapocheza na Mali ambao ndio vinara wa kundi hilo.

Wakati Eagles wakihitaji sare ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora, Brave Warriors watakuwa wakitafuta matokeo mazuri ili kumaliza ndani ya nafasi mbili za juu au kutinga kizingiti kinachofuata kama mmoja wa wamalizaji bora wa nafasi ya tatu.

Ni mchezo wa dau kubwa na unaohitaji kufanya uamuzi sahihi kuhusu timu gani utafanyia utabiri.

HABARI NA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA NAMIBIA.

Namibia wametiwa nguvu kwa kupatikana kwa mchezaji wao hatari Peter Shalulile. Nambibia walipata kipigo dhidi ya Bafana Bafana siku ya Jumapili jioni.

Baada ya mapambano yao, Petrus Shitembi na Absalom Limbondi huenda wasianze dhidi ya Eagles huku kocha Collin Benjamin akitumai kupata matokeo chanya.

KIKOSI CHA NAMIBIA KINACHOTAZAMIWA KUANZA: Kazapua, Nyambe, Amutenya, Haukongo, Hanamub, Petrus, Muzeu, Katua, Tjiueza, Hotto, Shalulile

HABARI NA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA MALI.

Kiungo wa Tottenham Hotspur Yves Bissouma anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuwekwa benchi katika mchezo uliopita dhidi ya Tunisia. The Eagles haitarajiwi kufanya mabadiliko mengi kutoka kwa timu iliyocheza na Carthage Eagles.

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA MALI KINACHOTAMIWA KUANZA: Diarra, Traore, Kouyate, Niakate, Sacko, Dieng, Bissouma, Haidara, Doumbia; Sinayoko, Koita

MATOKEO YA HIVI KARIBUNI, NAMIBIA NA MALI.

Hivi karibuni Namibia ilifungwa 4-0 katika mchezo wao wa Kundi E dhidi ya wapinzani wao wa Kusini mwa Afrika Bafana Bafana huku Mali na Tunisia zikitoka sare ya 1-1. The Eagles wataingia uwanjani wakiwa bora baada ya kushinda mechi zote mbili za kufuzu Afcon 2021, 1-0 na 1-2, mtawalia.

Popular Posts

Exit mobile version