AFCON

MAAJABU YA KOCHA WA MAURITANIA.

Published on

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Mauritania Mfaransa Amir Abdou jana amewashtua wengi baada ya timu yake kuipa kichapo timu ya Taifa ya Algeria [1-0] na kusonga mbele hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON 2023.

Kocha huyu kwenye AFCON ya mwaka 2021 alikuwa anakiongoza kikosi cha Comoro ambacho kiliacha alama kwenye michuano hiyo kikimpa kichapo Ghana cha goli 3-2.

Kama una kumbuka vyema kwenye mchezo dhidi ya mwenyeji wa mashindano hayo Cameroon, walikutwa na kadhia ya COVID 19 kabla ya mchezo huo, wakawapoteza magolikipa wake wote ikabidi mchezaji mmoja aingie langoni.

Amekuwa kocha wa malengo sana anapokuwa anaiongoza timu yake yoyote ile kwenye mashindano yote.

Amir Abdou baada ya mchezo aliweka wazi kuwa ulikuwa ni ushindi mgumu sana mbele ya Algeria, aliwaambia wachezaji wake wasiache chochote, wajitoe kwa asilimia zote hadi filimbi ya mwisho.

“Tunajisikia zaidi ya vizuri baada ya kupita hii hatua, niliwaambia wachezaji wangu wajitoe kwa asilimia zote huku wakiamini hadi kipyenga cha mwisho”.

“Tumeona kila kitu ambacho tuliongea na tumeziangalia timu zingine pia, hatimae tumefanikiwa kushinda dhidi ya timu ya Algeria”.

“Mmoja mmoja na kitimu, tumeonyesha ukomavu wetu hadi kuvuka hatua inayofuata, tutaanzia hapa”.

“Ni ushindi mgumu, upo kwenye kwenye nchi ambayo hauwajui watu wengi sehemu ambayo unapata matokeo na watu wanaenda kukushangilia katikati”.

“Wachezaji wamekuwa na mchezo wa historia kwao, niliwaambia jana kuwa wanapaswa kuandika majina yao kwenye vitabu vya historia kwenye mpira wa Mauritania na wamefanya hivyo”.

Popular Posts

Exit mobile version