Nyota wa zamani wa Manchester United na mshindi wa kombe la mataifa ya Afrika [AFCON] 2002 Eric Djemba Djemba amemshauri kocha wa Cameroon Rigobert Song kumuanzisha Onana kwenye mechi ya Leo ya 16 bora dhidi ya Nigeria.
Djemba Djemba anaamini Onana bado ni kipa bora zaidi kwenye kikosi cha Cameroon kuliko Ondoa, nyota aliyecheza mechi ya kwanza ya Cameroon na ya mwisho.
“Kuanzia mwanzo, Song alitakiwa kumwambia Onana aje tangu mwanzo au asije kabisa”.
“Kwasababu shirikisho la soka la Cameroon lilitoa ruhusa kwa Manchester United kusalia na nyota huyo na ndicho walichofanya, wangesema ajiunge na kikosi baada ya kuitwa tu”.
“Sasa hivi yupo na kikosi, na kiukweli ni golikipa mzuri kuliko Ondoa, huwezi kuwalinganisha hawa wawili”.
“Ni mmoja kati ya magolikipa bora Afrika anahitajika acheze, ni kitu cha ajabu kukaa benchi”, Alisema Eric Djembe Djemba.
Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United [42] amemtaja Mohamed Salah kama mchezaji bora Dunia na anaamini Misri inateseka bila nyota huyo.
“Salah ni moja ya wachezaji bora sio tu Afrika lakini Duniani”.
“Ni ngumu kuchukua kwasababu ndiye mchezaji nyota na ni mfungaji bora wa Liverpool”.
“Tumeona wachezaji vijana wameingia kwenye kikosi cha Misri labda tunaweza kuwaona wakiingia kutoka benchi”.
“Lakini kila mmoja anajua Misri hawafanyi vizuri wana hangaika, natumaini watafika nusu fainali na labda Salah anaweza akawa amepona”, Aliongeza Eric Djemba Djemba.