Ligi Nyingine

DE GEA KUTIMKIA SAUDIA.

Published on

Je, David de Gea hatimaye amepata klabu yake inayofuata? Al-Shabab wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili golikipa wa zamani wa Man Utd baada ya kutolewa Old Trafford majira ya kiangazi.

Golikipa wa zamani wa Manchester United na mchezaji huru David de Gea anaripotiwa kufanya mazungumzo na klabu ya Al-Shabab inayoshiriki Ligi ya Saudia.

De Gea aliachana na Mashetani Wekundu mwishoni mwa msimu uliopita, na kumaliza ushirika wa miaka 12 huko Old Trafford.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alionekana tayari kusaini mkataba mpya na klabu hiyo Juni mwaka jana, na kukatwa mshahara katika mchakato huo, lakini United walijiondoa kwenye mchakato huo na badala yake wakamsajili Andre Onana wa Inter. Baada ya hapo awali kuhusishwa na Al-Nassr na Newcastle United, Daily Mail linaripoti mazungumzo yanaendelea na Al-Shabab kuhusu uhamisho.

De Gea, ambaye aliichezea United mara 545, aliripotiwa kupewa mkono wa kwaheri huku Mashetani Wekundu wakitaka kipa ambaye alikuwa anajiamini zaidi akiwa na mpira miguuni mwake ili kuanzisha mashambulizi.

Wakati Onana aliyesajiliwa kwa pauni milioni 47.2 ($59.9m) ana ustadi zaidi kiufundi, bado kuna mjadala kwamba wababe hao wa Ligi Kuu ya Uingereza walifanya makosa kumruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania kuondoka katika viunga vya Old Trafford.

Katika msimu wa mwisho wa De Gea akiwa na United alishinda kipa bora wa msimu wa Ligi Kuu nchini Uingereza (EPL) baada ya kupata hati safi (clean sheets) 17 huku vijana wa Erik ten Hag wakimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi hiyo pendwa duniani. Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Mhispania huyo kutwaa tuzo hiyo kufuatia mafanikio yake msimu wa 2017/18 alipopata hati safi (clean sheets) 18.

Kwa vile De Gea ni mchezaji huru, hafungwi na dirisha la uhamisho la Januari ili kukamilisha dili hilo haraka iwezekanavyo. Baada ya kuwa bila klabu kwa zaidi ya miezi sita, mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid anaweza kuhitaji muda ili kurudisha kiwango chake baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu lakini ukweli kwamba Al-Shabab hawatacheza tena hadi katikati ya Februari hiyo inaweza kumsaidia kurejesha kiwango chake na kumruhusu kuzoea mazingira mapya.

Popular Posts

Exit mobile version