Inasemekana kuwa moja ya pambano kubwa zaidi katika hatua ya mtoano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 pale ambapo Taifa mwenyeji ambaye ni Ivory Coast itamenyana na mabingwa watetezi ambaye ni Senegal siku ya leo Jumatatu usiku.
TAARIFA YA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST.
Wenyeji walikuwa na bahati ya kufuzu, kuwa miongoni mwa timu zilizomaliza katika nafasi ya tatu bora, lakini watawezaje kuitetea bahati yao, hasa baada ya kuchapwa mabao 4-0 na Equatorial Guinea katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi A?.
Hata hivyo, wenyeji wana wachezaji wenye majina makubwa na macho yote ya watu wa Taifa la Ivory Coast yanatawazamia wao kusimama kidete dhidu ya mabingwa hao watetezi ambao wameshinda mechiz zao zote kwa asilimia 100 katika michuano hii ya Afcon inayoendelea huko nchini Ivory Coast.
KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST KINACHO TAZAMIWA KUANZA DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA SENEGAL.
Mabingwa hao watetezi ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kulitwaa taji la ubingwa katika michuano ya Afcon, wakiwa wamefunga mabao nane, wakiruhusu moja pekee na kutinga hatua ya robo fainali.
Mshambuliaji na mchezaji wa zamani wa Liverpool, Sadio Mane, beki na nahodha Kalidou Koulibaly na kipa Eduardo Mendy wote wanatarajiwa kuwa sehemu ya mchezo wao dhidi ya taifa mwenyeji.
KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA SENEGAL KINACHO TAZAMIA KUANZA DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST.
TAKWIMU ZA TIMU HIZI MBILI ZILIPOKUTANA MARA YA MWISHO.
Kwa kumbukumbu zilizo sawa zinaonesha timu ya Taifa ya Ivory Coast imekuwa ikipata matokeo mazuri zaidi ya Senegal mara nne ya mwisho kwa timu hizi kukutana. Ivory Coast ikishinda mara mbili dhidi ya mara moja ya Senegal huku mchezo mmoja ukimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Ivory Coast imefanikiwa kuziona nyavu za mpinzani wake mara saba (07) dhidi ya mara nne (04) kwa Taifa la Senegal.