AFCON

VITA YA FUNGAJI BORA AFCON.

Published on

Mbio za kusisimua katika kuwania kiatu cha dhahabu kwenye Afcon 2023. Dauda Sports inakuletea taarifa kuhusu wafungaji bora wanaoongoza kwa upachikaji mabao katika Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast.

Tukio hilo kubwa zaidi la mpira wa miguu barani Afrika lilianza Jumamosi, Januari 13, huku wachezaji wakijitokeza kwa kasi katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo inayoheshimika ya kiatu cha dhahabu.

Vincent Aboubakar wa Cameroon kwa sasa anashikilia tuzo hiyo, akiwa amefunga mabao manane katika mashindano ya 2021.

Swali: Nani atapita idadi hiyo ya mabao au kuchukua tuzo ambayo inashikiliwa na Vicent Aboubakar? . Dauda Sports inakuletea orodha ya wafungaji katika michuano hii mikubwa barani Afrika.

EMILIO NSUE (EQUATORIAL GUINEA) – 5.

Fowadi huyo wa CF Intercity mwenye umri wa miaka 34 alionyesha ukatili wake Alhamisi, Januari 18 baada ya kufunga hat-trick katika ushindi wa 4-2 wa Equatorial Guinea dhidi ya Guinea-Bissau katika mechi ya pili ya Kundi A.

Mshambuliaji huyo aliongeza mabao mengine mawili wakati timu yake ikiifunga Ivory Coast 4-0 katika mechi ya kundi A mzunguko wa tatu.

MOSTAFA MOHAMED (EGYPT) – 4.

Mshambuliaji huyo wa Misri sasa amefunga mabao mawili katika mechi nyingi za Kundi B akiwa na Mafarao.

Aliongeza la tatu huku Mafarao wakitoka sare ya 2-2 na Cape Verde na kulazimisha kuingia hatua ya 16 bora.

Mohamed alifunga bao lake la nne katika michuano hiyo wakati Misri ilipotoka sare ya 1-1 na DR Congo kwenye hatua ya 16 Bora lakini wakapoteza kwa mikwaju ya penati.

GELSON DALA (ANGOLA) – 4.

Dala alifunga mabao mawili dhidi ya Mauritania huku Angola ikishinda 3-2 katika mechi hii ya kusisimua.

Mchezaji huyo wa Angola alifunga mabao mengine mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Namibia katika hatua ya 16 bora.

CRISTOVAO ‘MABULULU’ PACIENCIA (ANGOLA) – 3.

Baada ya kufunga bao dhidi ya Algeria, Mabululu alifunga goli katika mechi ya mwisho ya Kundi D dhidi ya Burkina Faso timu yake ikishinda 2-0 na kutinga hatua inayofuata.

Alirejea tena kambani katika ushindi wa 3-0 katika hatua ya 16 bora dhidi ya Namibia.

BAGHDAD BOUNEDJAH (ALGERIA) -3.

Fowadi huyo mwenye uzoefu alifunga bao la kwanza katika sare ya 1-1 na Angola mnamo Januari 15, kabla ya kufunga mengine mawili na kuokoa pointi moja kwa Algeria dhidi ya Burkina Faso Januari 20.

MOHAMED BAYO (GUINEA) – 2.

Baada ya kufunga bao la kwanza katika Kundi C sare ya 1-1 na Cameroon, Bayo alifunga bao lake la pili la michuano hiyo dhidi ya Equatorial Guinea katika hatua ya 16 bora.

ADEMOLA LOOKMAN (NIGERI) – 2.

Mchezaji huyo anayeichezea klabu yake Atalanta ya nchini Italia alifunga katika kipindi chote cha pili wakati mabao yake mawili yalipoizamisha Cameroon 2-0 na kuipeleka Nigeria katika hatua ya 16 bora.

THEMBA ZWANE (AFRIKA KUSINI) – 2.

Mshambuliaji huyo wa Mamelodi Sundowns alifunga mabao mawili wakati Bafana Bafana ilipoichapa Namibia 4-0 mnamo Januari 21.

JORDAN AYEW (GHANA) – 2.

Winga huyo wa Crystal Palace alifunga mabao mawili kwa mikwaju ya penati katika sare ya 2-2 na Msumbiji katika mechi ya mzunguko wa tatu katika kundi.

LASSINE SINAYOKO (MALI) – 2.

Baada ya kupata bao la kwanza dhidi ya Afrika Kusini, Sinayoko alirudi kutikisa nyavu tena katika sare ya 1-1 ya Kundi E dhidi ya waarabu wa Tunisia.

LAMINE CAMARA (SENEGAL) – 2.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alikua mfungaji mdogo zaidi wa Senegal kwenye Afcon baada ya kufunga mabao mawili katika mechi ya ufunguzi ya Simba wa Teranga (Senegal) dhidi ya Gambia, katika mechi iliyochezwa hiyo Januari 15.

MOHAMMED KUDUS (GHANA) – 2.

Mshambuliaji wa West Ham United na timu ya Taifa ya Ghana alifunga mabao mawili katika sare ya 2-2 ya Black Stars dhidi ya Misri katika mechi ya mzunguko wa pili wa kundi B.

BETRAND TRAORE (BURKINA FASO) – 2.

Mshambuliaji Traore alifunga mabao yake mawili katika mechi mbili za mwanzo katika mzunguko wa kwanza na wa pili kwenye hatua ya makundi.

WACHEZAJI ZAIDI YA 50 BAO MOJA PEKEE.

Baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa katika soka la Afrika, kama vile Sadio Mane, Mohammed Salah, Achraf Hakimi, Victor Osimhen, Percy Tau na Hakim Ziyech wote wana bao moja katika mashindano haya ya Mataifa barani Afrika (AFCON).

Popular Posts

Exit mobile version