AFCON

16 BORA, MOROCCO vs. SOUTH AFRICA.

Published on

Morocco wanamenyana na washindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 1996 Afrika Kusini katika Uwanja wa Laurent Pokou leo siku ya Jumanne ifikapo saa tano usiku.

Wenyeji hao wa Afrika Kaskazini walikumbana na suluhu dhidi ya Congo katika hatua ya makundi, lakini uthabiti wao uling’aa walipopata ushindi katika mechi zao nyingine mbili, na kuwafanya kutinga katika hatua ya mtoano.

Kwa upande wa pili, Afrika Kusini ilijihakikishia nafasi ya kufuzu kwa hatua ya 16 kwa ushindi mmoja katika hatua ya makundi, ushindi wa ajabu wa 4-0 dhidi ya Namibia ambapo mabao mawili ya Themba Zwane yalihanikiza ushindi wa Bafana Bafana.

TAARIFA YA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA MOROCCO.

Noussair Mazraoui sasa ametimiza masharti ya kuchaguliwa dhidi ya Afrika Kusini, kuongeza nguvu kwa timu.

Katika safu ya ulinzi Romain Saiss na Nayef Aguerd wanatazamiwa kuanza pamoja. Katika safu ya ushambuliaji, Youssef En-Nesyri, ambaye hakuwepo katika ushindi wa mwisho dhidi ya Zambia, yuko tayari kurejea na kuongoza mashambulizi ya timu hiyo usiku wa leo.

Kwa bahati mbaya, timu hiyo itamkosa Sofiane Boufal, ambaye hayupo kutokana na majeraha, huku nahodha Hakim Ziyech akiwa na hati hati ya kucheza.

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA MOROCCO KINACHO TAZAMIWA KUANZA DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA AFRIKA KUSINI.

Bono; Hakimi, Aguerd, Saiss, Chibi; Amrabat; Ziyech, Ounahi, Amallah, Boufal; En-Nesyri.

TAARIFA YA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA AFRIKA KUSINI.

Afrika Kusini, kufuatia mechi yao dhidi ya Tunisia, ilikuwa na tatizo moja pekee la majeraha. Khuliso Mudau alibadilishwa baada ya kufunga goli.

Kwa kuzingatia kiwango kizuri katika mchezo uliopita, haitashangaza ikiwa Kocha Broos ataamua kutobadilisha kikosi iwapo wachezaji wake wote watakuwa fiti na wanapatikana.

Macho yote yatakuwa kwa straika Evidence Makgopa, ambaye ameanza kulaumiwa kwa kukosa umakini mbele ya lango.

Wakati huo huo, mchezaji nyota Percy Tau, ambaye alifunga penati dhidi ya Namibia, bado hajafunga katika mchezo uliopita pamoja na Themba Zwane, mchezaji mkongwe zaidi wa Bafana kambini, tayari ameshapachika mabao mawili.

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA AFRIKA KUSINI KINACHO TAZAMIWA KUANZA DHIDI YA MOROCCO.

Williams; Mudau, Kekana, Mvala, Modiba; Mokoena, Sithole; Zwane, Tau, Morena; Makkopa.

TAKWIMU ZA TIMU HIZI MARA YA MWISHO ZILIPOKUTANA.

Rekodi za timu hizi katika mechi tano za mwisho timu ya Taifa ya Morocco imeshinda mara nyingi zaidi ya Afrika Kusini, Morroco imeshinda mara mbili huku Afrika kusini ikishinda mara moja, huku timu hizo zikipata sare za kufungana katika michezo miwili.

Morocco imefunga jumla ya mabao saba (07) na Afrika kusini ikifanikiwa kuziona nyavu za timu ya Taifa ya Morocco mara sita (06).

Kwa takwimu hizo zinaonesha timu hizi mbili zina uwezo unaopishana kidogo, lakini kwa namna ambavyo timu ya Taifa ya Morroco imekuwa ikiingia na mipango mikakati tofauti tofauti kutokana na aina ya mpinzani wanayekutana nae, nafasi kubwa ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali iko upande wao.

South Africa 2 – 1 Morocco – 06/17/23

Morocco 2 – 1 South Africa – 06/10/22

South Africa 0 – 1 Morocco – 07/01/19

Morocco 1 – 1 South Africa – 10/12/13

Morocco 2 – 2 South Africa -01/27/13

Popular Posts

Exit mobile version