Makala Nyingine

RED EYES IMEITESA SIMBA KOMBE LA ASFC.

Published on

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba zinaeleza kuwa nyota takribani 10 wa kikosi hicho wanakumbwa na ugonjwa wa macho mekundu [Red Eyes] jambo lililopelekea kutokuwa sehemu ya kikosi kinachoikabili Tembo hii leo.

Kutokana na kuugua kwa nyota hao Simba imejikuta ikiingia uwanjani kuikabili Tembo kwenye mchezo wa ASFC ikiwa na wachezaji 15, 11 wakianza ndani na nyota wanne [4] wakiwa kwenye benchi la ufundi.

Kukosekana kwa nyota hao kumesababisha Shomari Kapombe kucheza eneo la kiungo baada ya nyota Che Marlone pia kupata ugonjwa huo.

Simba SC ina wachezaji wanne (4) tu kwenye benchi kwa maana ya watatu Pa Omar Jobe, Karabaka na Chasambi pamoja mlinda mlango Teru ukiachana na wachezaji walioanza leo mbele ya Tembo FC.

Kwa mujibu wa Taarifa zinasema kuwa ugonjwa huu umeenea takribani mikoa 17 nchini na unaambukizwa kwa njia ya kugusana.

Kama ikitokea mgonjwa akagusa majimaji ya macho yake halafu akamgusa mwingine na yeye akagusa macho yake basi atakuwa ameambukizwa ugonjwa huo.

Ili kupunguza madhara kwa klabu hiyo ya Simba wameamua kuwatenga nyota walioambukizwa ugonjwa huo ili usije ukawaathiri na nyota wengine waliosalia kwenye kikosi hicho.

Popular Posts

Exit mobile version