Makala Nyingine

TSHABALALA AFURAHI KUKUTANA NA BEKI WA STARS.

Published on

Michuano ya AFCON 2023 imekuwa fursa kwa Mohamed Hussein Zimbwe ‘Tshabalala’ kukutana na legend wa Afrika Kusini Siphiwe Tshabalala ambaye kwa kiasi kikubwa ndio mchezaji aliyemvutia zaidi Zimbwe Jr kuupenda mchezo wa soka.

Ndoto ya Mohamed Hussein kukutana na Tshabalala ilitimia huko Korhogo, Ivory Coast ambako Taifa Stars ilicheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi F dhidi ya DR Congo.

Licha ya Taifa Stars kushindwa kufuzu hatua ya 16 Bora ya AFCON 2023 lakini kwa Mohamed Hussein huenda alikuwa na furaha ya kukutana na ‘Role model’ wake Siphiwe Tshabalala ambaye ni miongoni mwa wachezaji wakongwe walioalikwa na CAF.

Tshabalala ndio mchezaji aliyefunga goli la kwanza kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2010 kwenye mchezo kati ya Afrika Kusini dhidi ya Mexico.

Mohamed Hussein ambaye aliwahi kutumia jina la Tshabalala kwenye jezi yake, amesema amefurahi kukutana na nyota ambaye alimfanya aupende mchezo wa mpira wa miguu Siphiwe Tshabalala aliyewahi kuiwakilisha Afrika Kusini kwenye Fainali tatu za AFCON [2006, 2008 na 2013].

“Hatimaye nimekutana na mtu aliyenivutia na kunifanya niupende zaidi mchezo huu [mpira wa miguu]. Alinifanya niandike jina lake kwenye jezi yangu. Mtumiaji wa mguu wa dhahabu na mfungaji wa goli la kwanza la Kombe la Dunia 2010″, Mohamed Hussein, nyota wa Stars na klabu ya Simba.

Mohamed Hussein alikuwa na umri wa miaka 13 wakati Tshabalala anaandika historia kwenye ardhi ya Afrika Kusini. Tangu hapo akaamua kuchangua ‘Tshabalala’ kuwa jina lake la utani na alikuwa anatamani siku moja akutane na nyota huyo.

“Nikiwa Afrika Kusini mara kadhaa niliambiwa kuhusu kijana huyu wa Tanzania [Mohamed Hussein]. Nimefurahi sana hatimaye nimekutana na Mohamed”, SiphiweTshabalala.

Popular Posts

Exit mobile version