Mashabiki wa soka nchini Nigeria wameilalamikia klabu ya Napoli kwa kutokuonyesha ushirikiano kwa nyota wa Victor Osimhen katika kipindi ambacho yupo kwenye fainali za mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast.
“Napoli namna wanavyoomba ndio wanafanya Nigeria isimrudishe Osimhen mapema, nenda kaangalie wame “post” namna walivyo na furaha kwa urejeo wa Anguissa wa Cameroon, wameandika “Tabiri nani amerejea☺️”.
“Kila klabu ina utamaduni wake”, alisema shabiki mwingine wa Nigeria.
“Wanajua hawawezi kubaki nae”, alizungumza shabiki wa tatu.
“Cha msingi ni kuwa wana mlipa mshahara wake, hicho ndio cha msingi”, shabiki wa nne alinena.
“Ni klabu ya ajabu sana, tunamshukuru Mungu anaondoka, klabu itashuka uwezo”, alimaliza shabiki wa tano wa Nigeria.
Napoli tangu mashindano haya yaanze rasmi January 13 haijampost Victor Osimhen kumtakia heri katika michezo yake kama ambavyo klabu kadhaa kutoka Barani Ulaya zinavyowapost nyota wale wanaoshiriki fainali hizo.
Nigeria imefuzu hatua ya nusu fainali na itamenyana na Afrika Kusini Jumatano hii na kama wakifuzu basi Victor Osimhen atakuwa na muda mwingine wa kuendelea kusalia Ivory Coast.