Chelsea jana ilichezea chuma nne [4-2] kutoka klabu ya Wolves kwenye mchezo wa EPL, kocha mkuu wa kikosi hicho Mauricio Pochettino amewaomba msamaha mashabiki wa klabu hiyo na kusema hakuna aliyebora kwasasa.
“Nataka kuwaomba msamaha mashabiki, ilikuwa siku ngumu kwa kila mmoja, kwa wachezaji, kwetu sisi lakini pia kwa mashabiki”.
“Tumefanya makosa ambayo hautakiwi kuyafanya kwenye Ligi kuu lakini wote tumesikitishwa sana”.
“Tumesikitishwa sana lakini mwisho wa siku tunahitajika kupambana pamoja kama tunavyoihisi presha sasa”.
“Sitaki kuja hapa na kusema kuwa mimi ni bora, kwa wakati huu hatuendani na historia ya klabu hii”.
“Wote hatuko bora sana [Sio wachezaji tu], na huo ndio uhalisia, mimi pia, kitu tunachokionyesha ni kuwa hatujawa bora, hakuna ambaye yupo salama”, alisema Pochettino.
Hadi hivi sasa klabu hiyo ipo nafasi ya kumi na moja [11] ya msimamo wa Ligi kuu nchini England ikiwa imekusanya alama 31 kwenye michezo 23 iliyocheza.
Wolves baada ya ushindi wa jana imepanda hadi nafadi ya kumi [10] ya msimamo ikiwa na alama 32 katika michezo 23 ya Ligi kuu EPL iliyocheza msimu huu.