NBC Premier League

YANGA INAIONEA DODOMA JIJI LIGI KUU TANZANIA BARA.

Published on

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja kuchezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Yanga.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa moja [19:00] usiku, hizi ni takwimu za timu zote mbili Yanga na Dodoma Jiji kuelekea mchezo wao wa leo.

  • Yanga inashika nafasi ya pili [2] ya msimamo wa Ligi kuu ikiwa na alama 31 ikiwa imecheza michezo 12, kama ikishinda hii leo itafikisha alama 34 zitakazoifanya ikwee kileleni mwa msimamo wa Ligi na kuiacha Azam yenye alama 31 hadi hivi sasa ikiwa imecheza michezo 13.
  • Dodoma Jiji inashika nafasi ya saba [7] ya msimamo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara ikiwa na alama 18 ikiwa imecheza mechi 13, ikishinda hii leo itafikisha alama 21 na kukwea hadi nafasi ya nne [4].
  • Yanga imeshinda michezo kumi [10], imepoteza mmoja [1] na imetoka sare mchezo mmoja [1], hadi hivi sasa.
  • Dodoma Jiji imeshinda michezo mitano [5], wamepoteza michezo mitano [5] na wametoa sare michezo mitatu [3].
  • Yanga imefunga jumla ya magoli magoli 31 na kuruhusu magoli sita [6] pekee huku Dodoma Jiji imefunga magoli 12 na kufungwa 13.
  • Yanga imecheza michezo sita [6] ikiwa mwenyeji wa mchezo na imeshinda mechi zote, imevuna alama 18, imefunga magoli 20 na kuruhusu magoli matatu [3] pekee.
  • Dodoma Jiji ikiwa ugenini imecheza mechi saba [7], imevuna alama Saba [7], imeshinda michezo miwili [2], imetoa sare mchezo mmoja [1] na imepoteza michezo minne [4], imefunga magoli sita [6] na kuruhusu magoli tisa [9].
  • Timu hizi zimekutana mara sita [6] kwenye michezo ya Ligi kuu Tanzania Bara, Yanga imeshinda mara tano [5], mara moja [1] sare.
  • Yanga imeifunga Dodoma Jiji magoli 15 na Dodoma Jiji imeifunga Yanga magoli matatu.
  • Mchezo wa mwisho kwa timu hizi kukutana Yanga ilishinda goli 4-2.

Leo ni mchezo mwingine kwa Yanga wakitamani kurejea kwenye ubora wao baada ya kulazimishwa sare mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.

Popular Posts

Exit mobile version