Mlinda lango wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini Ronwen Williams ameisifia safu yake ya ulinzi kwa kazi kubwa wanayoifanya kwenye fainali hizi za AFCON.
Ronwen amekuwa na wakati mzuri kwenye kikosi cha Bafana Bafana ambapo katika michezo mitano [5] ameondoka na hati safi [Cleansheet] tatu [3].
“Washambuliaji na viungo wanacheza vizuri sana lakini eneo la ulinzi wamekuwa bora zaidi kwenye mashindano haya”, Alisema Williams.
“Tunajua utakuwa mchezo mgumu dhidi ya Nigeria lakini tunauangalia zaidi huo mchezo”.
Afrika kusini itashuka dimbani hii leo saa 12 Jioni kuikabiki timu ya Taifa ya Nigeria kwenye hatua ya nusu fainali.