AFCON

MALALAMIKO HUGO ANALIPWA PESA KUBWA BILA KAZI

Published on

Viongozi wa bodi ya Ligi kuu nchini Afrika Kusini wametoa lawama zao kwa shirikisho la soka nchini Afrika Kusini kuhusu kiwango cha pesa anacholipwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Hugo Broos kuwa ni kikubwa mno tofauti na kazi anayofanya.

Broos analipwa R750,000 sawa na USD 50,000 ambayo kwa pesa ya kitanzania Million 127 kiasi ambacho ni kikubwa tofauti na kile walichokuwa wanapokea makocha waliomtangulia Stuart Baxter na Pitso Mosimane waliokuwa wanapokea Million sita [R50,000].

Hata hivyo shirikisho la soka nchini Afrika Kusini limemkingia kifua kocha huyo ambaye ni mshindi wa fainali za mataifa ya Afrika mara moja.

Afrika Kusini jana iliondoshwa kwa mikwaju ya penalty dhidi ya Nigeria kwenye hatua ya Nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa Barani Afrika, kocha Broos amesema wamecheza vyema kwenye mashindano haya.

“Ni huzuni kwa kila mmoja kwasababu tunahisi tumechezaa mchezo mzuri, sio leo tu, tumecheza AFCON bora sana”, Alisema Hugo.

“Na ninajivunia sana hilo, najivunia wachezaji wangu, tumesikitishwa ndio lakini tunajivunia kile walichokifanya, kile walichokionyesha, sio leo tu nafikiri napaswa kujivunia pia kama kocha”.

“Huo ndio mpira, nafikiri tunafaswa kufikiria zaidi namna ambavyo tumecheza michuano hii ya AFCON, na najua kuwa kila mmoja ameifahamu Afrika Kusini sasa kama timu inayocheza mpira, na hicho ndio kitu cha msingi”, Alimalizia Hugo Broos.

Afrika Kusini iliondoshwa na Nigeria hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya Penalty 4-2 hapo jana.

Popular Posts

Exit mobile version