Klabu ya Napoli imeichapisha picha ya Victor Osimhen kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii baada ya nyota huyo kufuzu hatua ya fainali ya michuano ya mataifa ya ya Afrika inayoendelea huko nchini Ivory Coast.
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Napoli kuchapisha picha ya pongezi kwa nyota huyo tangu michuano hii ilipoanza kitu ambacho kimewafanya mashabiki wa soka nchini Nigeria kuijia juu klabu hiyo.
Mashabiki hao kwa nyakati tofauti wamemtaka nyota wao Victor Osimhen aondoke kwenye klabu hiyo wakiamini kuwa hawamtendei haki kama ambavyo nyota wengine wamefanyiwa na klabu zao kwenye fainali hizi za AFCON.
“Walikuwa wapi toka zamani kumpost ndio waje wafanye hivyo leo? Hadi tuwaseme kwenye mitandao?”, Alisema shabiki mmoja.
“Sijui nini mnakiwaza mmeanza kujipendekeza sasa naona”, alizungumza shabiki mwingine.
“Bora uondoke tu ndugu yetu, maana wanaonyesha kukutenga waziwazi”, aliongeza shabiki mwingine.
“Hivi mnajisikiaje kumpost baada ya kufuzu fainali ? Mmempost kishingo upande tunajua”, aliongeza shabiki mwingine.
Nigeria imefuzu hatua ya fainali kwenye fainali za mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Ivory Coast na sasa itakutana na mwenyeji wa michuano hii timu ya Taifa ya Ivory Coast.
Victor Osimhen ni kwa mara ya kwanza anashiriki michuano hii mikubwa Barani Afrika na anafika fainali ambayo itapigwa jumapili, February 11, 2024.