NBC Premier League

MWAGALA: MATOKEO YA SIMBA YALITUUMIZA.

Published on

Kikosi cha Tabora United leo kitaanza maandalizi  kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Namungo ya Ruangwa Mkoani Lindi utakaochezwa Februali 11 katika Uwanja wa Alhasan Mwinyi Mjini Tabora.

Tabora United Chini ya Kocha Mkuu Goran Copunovic wataingia kwenye mazoezi jioni ya leo ikiwa ni siku moja tangu ilipotoka kupoteza mchezo wake dhidi ya Simba Februali 06 mwaka huu kwa magoli manne kwa bila.

 Tabora United baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Simba Kocha Goran alitoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji na leo hii Timu inaingia tena kwenye uwanja wa mazoezi kwa ajili ya kujiweka vizuri ili kumaliza mzunguko wa kwanza siku ya Jumapili.

­” Tumetoka kupoteza mchezo muhimu na Simba tukiwa kwenye uwanja wetu wa nyumbani matokeo ambayo yalimuumiza kila mmoja wetu, lakini tayari tumeshamaliza mchezo huo kikubwa kama Timu tunaangalia nafasi nyingine ambayo tunayo kwa Namungo”.

“Tunajua kabisa huu mchezo hautakuwa mwepesi kutokana na kwamba Namungo wanatimu nzuri, benchi zuri la ufundi lakini tunakwenda kwenye uwanja wa mazoezi kujiandaa ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi makosa ambayo yalijitokeza kwenye mchezo uliopita lakini pia ikumbukwe kwamba Timu bora sikuzote haipotezi mchezo mara mbili”.

“Hata hivyo kwa upande wa Afya za wachezaji wote wapo vizuri na kwamba kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo unaokuja na kwamba  mashabiki na Watanzania wote tunawaomba waendelee kutuunga mkono kwenye michezo yetu ya nyumbani na ile ya ugenini kwa lengo la kufanya vizuri”.
-Alisema Afisa habari wa Tabora United, Christina Mwagala.

Tabora United ipo kwenye nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi kuu ya NBC soka Tanzania bara ikiwa na jumla ya alama 15 na imecheza michezo 14  hivyo tunaendelea kuwasihi mashabiki zetu wasiwe na hofu na msimamo huo kwakuwa tunaamini tutatoka na kupanda kwenye nafasi za juu.

Popular Posts

Exit mobile version