Rais wa shirikisho la soka Barani Ulaya Aleksander Ceferin ametangaza kuwa hatashiriki uchaguzi wa nafasi hiyo utakaofanyika mwaka 2027, japo sheria inamruhusu kurejea tena kwenye nafasi hiyo.
Ceferin amesema kuwa sababu kubwa inayomfanya asitake tena kurudi kwenye nyadhifa yake ni za kifamilia lakini pia anazipisha damu changa ziongoze shirikisho hilo.
“Sababu ni kuwa baada ya muda shirikisho linahitaji damu mpya, lakini kubwa ni kuwa nilikuwa mbali na familia yangu kwa miaka saba sasa na nitakuwa mbali nao kwa miaka mitatu ijayo tena,” alisema Aleksander akiwa Paris.
Aleksander Ceferin [56] raia huyo wa Slovenia atalitumikia shirikisho hilo kwa miaka 10 hadi itakapofika mwaka 2027.