Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja kupigwa jijini Mwanza kati ya Simba dhidi ya Azam FC majira ya saa 10:00 Jioni.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa CCM Kirumba na kuelekea mchezo huu hizi ndizo takwimu pindi timu hizi zinapokutana.
Mechi – 20
Simba Ushindi – 7
Azam Ushindi – 5
Sare – 8
Azam imeshinda michezo yake yote mitano [5] ya mwisho ya Ligi, ipo nafasi ya pili [2] na Simba imeshinda michezo mitatu [3] na sare mbili [2], ipo nafasi ya tatu [3] ya msimamo.
Msimu huu klabu ya Azam FC imepoteza michezo miwili [2] na kutoka sare mchezo mmoja [1], imeshinda michezo kumi [10] katika michezo 13 iliyocheza.
Simba imepoteza mchezo mmoja [1] na sare michezo miwili [2], na imeshinda michezo tisa [9] katika michezo 12 iliyocheza msimu huu.
Simba imefunga magoli 28, imeruhusu magoli 13 na Azam imefunga magoli 35 na kuruhusu magoli kumi [10] msimu huu.
Mechi ya leo itaamua timu ipi ishike nafasi ya pili na kivyovyote vile nafasi ya kwanza haitaguswa na yoyote tofauti na Yanga vinara.