AFCON

RONWEN ANASTAHILI KUWA GOLIKIPA BORA AFCON 2023.

Published on

Timu ya Taifa ya Afrika Kusini jana imeibuka na ushindi katika mchezo wa kutafuta nafasi ya tatu kwenye fainali za mataifa ya Afrika [AFCON 2023] dhidi ya DR Congo.

Afrika Kusini na Congo DR zilitoshana nguvu ya 0-0 ndani ya dakika 90 na baadae changamoto ya mikwaju ya penalty ikafuata ili kujua nani ataibuka kuwa mshindi wa tatu wa fainali hizo zinazoendelea nchini Ivory Coast.

Afrika Kusini iliibuka na ushindi wa penalty 6-5 na mlinda lango wa klabu ya Mamelodi Sundowns na timu ya Taifa ya Afrika Kusini akiibuka shujaa kwa mara nyingine katika hatua hii baada ya kuokoa michomo miwili.

Takwimu za golikipa wa Afrika Kusini kwenye mashindano ya AFCON mwaka huu zimekuwa bora sana.

  • Mechi 7
  • Cleansheet 5
  • Ameokoa penalty 6 kwenye upigaji wa penalty mechi mbili.

Kama golikipa wa Nigeria Stanley Nwabali atashindwa kumaliza na hati safi [Cleansheet] kwenye mechi ya fainali basi Ronwen anaweza kuwa golikipa bora wa mashindano.

Baada ya mchezo huo kumalizika mlinzi wa klabu ya St. Ettiene na timu ya Taifa ya Congo DR, Dylan Batubinsika alitajwa kuwa nyota wa mchezo huo kutokana na kiwango bora alichokionyesha.

Hata baada ya kukosi kombe la AFCON nyota huyo amesema mashindano haya yalikuwa bora kwa upande wao.

“Nimefurahishwa na kombe hili, namshukuru Mungu kwa hili, nadhani tunapaswa kujivunia shindano letu, tumecheza vizuri na tutachukua mazuri kwenye hii safari, ni wachache waliotegemea sisi kufika hapa na ni kitu kizuri kwaajili ya kuijenga kesho yetu”, Alisema mlinzi huyo.

“Nitakumbuka mazuri kwenye safari yetu, kumbukumbu yangu bora inasalia kuwa ushindi dhidi ya Misri, ilikuwa mechi ngumu sana lakini tulipata ushindi mbele ya timu bora”, Alimaliza nyota huyo.

Popular Posts

Exit mobile version