NBC Premier League

JKT YAAHIDI KUMCHAPA SIMBA MECHI YA KESHO.

Published on

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo kati ya JKT Tanzania wakiwaalika klabu ya Simba.

JKT Tanzania kwa mara ya kwanza watautumia uwanja wao wa nyumbani Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar Es Salaam kwenye mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuufanyia marekebisho.

Kuelekea mchezo huo kocha wa magolikipa wa klabu ya Simba Daniel Cadena amesema atawakosa nyota wake wawili Aubin Kramo na Willy Onana kutokana na kuwa majeruhi huku wengine wakiendelea kuwa tayari kwaajili ya mchezo huo.

“Maandalizi yamekamilika, wachezaji wote wapo vizuri isipokuwa Kramo na Onana ambao ni majeruhi, lakini wengine wote wapo tayari kwaajili ya mchezo,” Alisema Cadena.

Kwa upande mwingine Cadena ameutaja mchezo huo kuwa utakua mgumu kwasababu ya JKT Tanzania kuhitaji kujinasua kutoka kwenye daraja ambalo timu hiyo ipo.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu, lakini tunachikihitaji ni ushindi na tunazihitaji alama zote tatu.”

“Utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia wapinzani wetu hawapo kwenye nafasi nzuri lakini tupo tayari kuwakabili.”- Kocha Daniel Cadena

Kwa upande wa JKT Tanzania kupitia kwa kocha wao msaidizi George Mketo wamesema wao wanahitaji kuufungua uwanja wa ushindi dhidi ya Simba licha ya ubora walionao wapinzani wao.

“Tunahitaji kuufungua Uwanja wetu vyema, na mwanzo wa mchezo wetu dhidi ya Simba naamini tutacheza vizuri zaidi kwenye michezo mingine inayofuata”.

“Tunahitaji kufanya vizuri kwasababu ni mechi ya kwanza kucheza kwenye uwanja wetu wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni na ni mechi ya mwisho kwenye mzunguko wa duru la kwanza”, Alisema George.

Mchezo wa JKT Tanzania na Simba utapigwa saa 10:00 Jioni na utakuwa mchezo wa mwisho kwa JKT Tanzania kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi.

Popular Posts

Exit mobile version