Timu za Taifa za Wanawake za Tanzania

TWIGA STARS INAJIWINDA NA AFRIKA KUSINI KUFUZU OLYMPIC.

Published on

Timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania “Twiga Stars” ipo kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu michuano ya Olympic inayotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa kwenye Jiji la Paris dhidi ya timu ya Taifa ya Afrika Kusini.

Mchezo wa kwanza utapigwa February 23 mwaka huu katika uwanja wa Azam Complex uliopo jijini Dar Es Salaam, kabla ya kwenda kurudiana tena nchini Afrika Kusini.

Kocha mkuu wa kikosi cha Twiga Stars Bakari Shime amesema maandalizi yao yanaenda vizuri na anatarajia kukaa na vijana wake kambini kwa takribani siku kumi kabla ya mchezo dhidi ya Afrika Kusini.

“Matayarisho kwaajili ya mchezo wetu wa kufuzu mashindano ya Olympic dhidi ya Africa Kusini yameanza rasmi tangu juzi, tutakuwa na kambi hii kwa takribani siku kumi kabla ya mchezo dhidi ya Afrika Kusini”.

“Ni mategemeo yetu kuwa tutafanya vizuri, kikubwa ni kuhakikisha matayarisho yanaenda vizuri, na kuweza kuwa na kikosi imara na kupata alama kwenye mchezo huu”.

“Ni hatua mbili zimebakia kwaajili ya kupata nafasi ya kufuzu mashindano haya ya Olympic”, Alisema Bakari Shime.

Twiga Stars imeweka kambi kwenye kituo cha ufundi cha TFF kilichopo Kigamboni, Jijini Dar Es Salaam na michuano hiyo ya Olympic itafanyika majira ya joto mwaka huu nchini Ufaransa kwenye Jiji la Paris.

Popular Posts

Exit mobile version