Top Story

NSUE: SHIRIKISHO LIMEKULA PESA YA TIMU YA TAIFA.

Published on

Nahodha wa timu ya Taifa ya Equatorial Guinea Emilio Nsue baada ya kufungiwa na shirikisho la soka la nchi hiyo ametoa shutuma nzito kwa shirikisho la soka la nchi hiyo akidai wamekula pesa iliyokuwa kwaajili ya timu ya Taifa.

Nsue alikuwa na kiwango bora sana kwenye fainali za mataifa ya Afrika baada ya kuibuka kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo ya AFCON 2023 iliyomalizika nchini Ivory Coast kwa kufunga magoli matano [5], huku bingwa akiwa mwenyeji Ivory Coast.

“Shirikisho letu la Mpira (Equatorial Guinea) walizunguka kwa watu Mashuhuri na wenye Fedha wakawaambia waichangie Timu ya Taifa iliyopo AFCON lakini hatukuona kazi ya pesa hizo, hata jezi za Timu ya Taifa tukiwa kambini tulifua sisi wenyewe”.

“Naumia kwasababu ile sio Timu yetu pekee ni Timu ya wote lakini mzigo wote walituachia sisi na bado wameona haitoshi wakaamua kunifungia kisa nasema ukweli”.

“Pesa zote mlizochanga kwaajili yetu tukiwa Ivory Coast mmetapeliwa, hatujaona faida yake na zimeliwa na maofisa mliowaamini ndani ya Shirikisho.”

  • Mshambuliaji wa Timu ya Taifa la Equatorial Guinea, Emilio Nsue.

Mara kadhaa mashirikisho ya soka Barani Afrika yamekuwa yakilaumiwa mara kadhaa kuhusu rushwa na matumizi mabaya ya pesa ambazo zinatengwa kwaajili ya timu za Taifa.

Popular Posts

Exit mobile version