Nyota wa klabu ya Inter Miami na timu ya Taifa ya Argentina Leonel Messi ameweka wazi kuwa tuzo yake ya nane ya Ballon D’or ataipeleka kuhifadhiwa kwenye jumba la makumbusho la klabu ya Barcelona.
Tuzo zake saba tayari zipo kwenye jumba la kumbukumbu la klabu hiyo ya Barcelona na E- Noticies wameweka wazi kuwa tuzo ya nane pia inakuja.
Messi aliwahi kunukuliwa akisema;
Kila kitu ninachomiliki kipo Barcelona kwenye jumba la makumbusho, Ballons d’Or, kiatu cha dhahabu [Golden Boots] na kila kitu.
Leonel Messi, nyota wa zamani wa Barcelona.
Messi amebeba tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia mara nane akiandika historia ya kuwa mwanasoka aliyebeba mara nyingi zaidi tuzo hiyo, tuzo ya nane ameibeba msimu huu akimshinda mshabuliaji wa Manchester City na timu ya Taifa ya Norway Erling Braut Haaland.
Messi pia amebeba tuzo ya Golden Boot mara sita kwenye historia akishikilia rekodi ya kubeba kiatu hicho cha dhahabu mara nyingi, akifanya hivyo mara sita huku mpinzani wake wa karibu Cristiano Ronaldo akiwa nafasi ya pili.