Mshambuliaji wa klabu ya CR Belouizdad Lamin Jallow baada ya kutua Tanzania ameweka wazi kiwa klabu wanayoenda kucheza nayo [Yanga] ni timu kubwa kama ilivyo kwa Mamelodi Sundowns na Al ahly.
Nyota huyo raia wa Gambia ameeleza kuwa hali ya hewa ya joto kwao sio changamoto kwani Asilimia kubwa ya nchi za Afrika hali ya hewa inaendana.
“Tunafahamu Yanga ni kubwa kama zilivyo Al Ahly au Mamelodi Sundowns na ndio maana wachezaji wote tuliokuja kwaajili ya mchezo huu tuna ari ya kutafuta ushindi wa wa kihistoria hapa Tanzania.”
“Hali ya hewa kwetu sio changamoto, unajua Afrika ni kama eneo moja, Mimi nimezaliwa Gambia na leo ndio mara yangu ya kwanza kufika ndani ya Tanzania lakini najihisi kama vile nipo kwetu.”
Maneno ya mshambuliaji wa CR Belouizdad, Lamin Jallow baada ya kutua Tanzania.
CR Belouizdad itacheza dhidi ya Yanga siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa moja jioni.
Mshindi kwenye mchezo huu atakuwa na nafasi nzuri ya kufuzu hatua inayofuata ya robo fainali huku kundi lao likiwa wazi kwa timu zote nne kupata nafasi ya kufuzu.
Msimamo.
Al Ahly ———- Pts 6
CR Belouizdad — Pts 5
Yanga ———— Pts 5
Medeama —— Pts 4.