Klabu ya Yanga imetangaza kuingia kandarasi na Kampuni ya Hero kwa mwamvuli wa Kampuni ya Karimujee Mobility nchini, Hero ni Kampuni watengenezaji wa pikipiki ya nchini India ambayo inapatikana kwenye nchi 40 Duniani.
Kutokana na kandarasi hili Yanga SC itavuna zaidi ya Milioni 300 awamu ya kwanza lakini pia itapata Gawio kupitia matawi ya Yanga SC ambao ndio watakuwa wateja wakubwa wa pikipiki hizi za Hero.
Akizungumza wa wanahabari Rais wa klabu ya Yanga Eng. Hersi Said amesema klabu hiyo itaingiza kiasi cha Million 300 kwa miezi 18.
“Leo tumeingia makubaliano na kampuni ya Karimjee Mobility kupitia kampuni ya Hero ambayo inatengeneza pikipiki na kusambaza”.
“Kampuni ya Hero inatajwa kuwa kampuni namba 1 duniani kwa biashara hiyo. Kampuni hii kutoka India inafanya biashara mataifa zaidi ya 40. Young Africans SC itapata kiasi cha Tsh Milioni 300 kutoka kwenye mkataba huu katika kipindi cha miezi 18”
- Rais wa Young Africans SC Eng. Hersi Said.
“Mkataba huu utaruhusu kwa matawi yetu ya Klabu kupata posho kwenye mauzo ya pikipiki hizo. Kwahiyo kila tawi linapaswa kuhakikisha biashara hii inakuwa kwa kasi. Hivyo basi kila mwananchi pikipiki yako ya kununua ni Hero na pikipiki ya kutumia ni Hero” Eng.Hersi Said.
Afisa Habari wa klabu ya Yanga Ally Shaban Kamwe ameeleza kuwa watu 10 wa mwanzo kununua pikipiki hizo watapata ofa mbalimbali ikiwemo Bima.
“Watu 10 wa kwanza kununua Hero watapata huduma ya pikipiki (services) mara tatu bure. Vile vile wanatoa bima ya dereva na mtaji wake. Utajipatia vile vile helmet yenye nembo ya Young Africans SC” Ally Kamwe