CAF Champions League

GAMONDI: TUMEJIANDAA KUSHAMBULIA MECHI YA KESHO.

Published on

Klabu ya Yanga kesho inatarajia kushuka dimbani kuikabili klabu ya CR Belouizdad ya nchini Algeria kwenye mwendelezo wa michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika.

Yanga na CR Belouizdad zote kwa pamoja zina alama sawa kwenye msimamo wa kundi D ikiwa kila timu ina alama tano, huku kinara wa kundi hilo Al Ahly akiwa na alama sita.

Kuelekea mchezo wa Leo klabu ya Yanga imeweka wazi kuwa mchezo wa kesho hautakuwa mchezo rahisi kwani kila timu inahitaji ipate matokeo ili ijiweke kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali.

Yanga chini ya Miguel Gamondi hadi hivi sasa imecheza michezo minne [4] kimataifa na imeshinda mchezo mmoja, imetoa sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja, ikumbukwe mchezo wa kwanza dhidi ya CR Belouizdad Yanga ilipoteza kwa goli 3-0.

Nahodha msaidizi wa klabu ya Yanga Dickson Job pia ameeleza kuwa mchezo wa kesho utakuwa na presha kubwa lakini wamejiandaa kushambulia na kuondoka na alama zote tatu.

Miguel kwa upande wake pia amesema mchezo wa kesho ni maalumu kwaajili ya kupata alama tatu na wamejipanga kushambulia ili waweze kupata matokeo.

MIGUEL GAMONDI – KOCHA YANGA.

Mchezo utakuwa mgumu na utakuwa ni mchezo wenye mbinu nyingi hasa wakati gani wa kushambulia na wakati gani wa kujilinda na tumeyafanyia kazi maeneno yote mawili na kuhakikisha tutatumia vizuri kila nafasi tutakayoipata kwenye mchezo wa kesho.

Ni mchezo mkubwa na wa aina yake, lakini kwetu sisi ni mchezo ambao tunatakiwa kushinda kwa namna yoyote ile ili tuweze kusonga mbele, Tumefanya maandalizi mazuri na akili yetu yote inaangalia mchezo wa kesho.

DICKSON JOB – NAHODHA MSAIDIZI YANGA.

Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho, mwanzo lengo lilikuwa ni kuingia hatua ya makundi baada ya muda mrefu lakini sasa lengo letu kwa pamoja ni kupambana na kusonga mbele zaidi kwa kila mchezo uliokuwa mbele yetu.

Pacome hana presha yoyote anajua umuhimu wa mchezo wa kesho na wachezaji wote tuko nyuma yake kumpa sapoti kwenye siku yake hii kubwa kama wachezaji wengine ambao wametangulia. Wote tutapewa mechi na hii ni heshima kubwa sana kwetu.

Hamasa zinazoendelea ni nzuri na sisi kama wachezaji tunaziona, na kuna muda zinatuongezea kitu kuelekea mechi na kupambana, lakini kuna muda mwingine zinatupa uoga yaani zinaogopesha.

Popular Posts

Exit mobile version